Wanawake wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamefanya utalii wa ndani kwa kutembelea maanguko ya maji ya mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani afrika kwa mita 235 kama sehemu ya mwendelezo wa maadhimisho ya mwanamke duniani.
Wakiongea katika nyakati tofauti wamesema wamelazimika kutembelea maeneo hayo ili kujifunza na kuona mandhari ya hifadhi ya mazingira ya Mto Kalambo na kuipongeza serikali kwa kuboresha miundombinu katika eneo hilo.
Afisa utalii hifadhi ya mazingira Kalambo kutoka wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Rose Aloice, amesema huo ni mwendelezo wa kampeni ya uhamasishaji wa makundi mbalimbali ya kijamii kufanya utalii wa ndani kila mwezi ili kujifunza na kuona mandhari ya hifadhi hiyo.
Hata hivyo maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa ngazi ya wilaya yalifanyika Machi 8, 2025 katika eneo la Mwimbi na kushirikisha makundi mbalimbali ya kijamii yakiwa na kauli mbiu isemayo ‘’Wanawake na wasichana 2025;Tuimarishe haki , Usawa na uwekezaji .
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.