Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo imeanzisha mpango maalumu wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu na matumizi sahihi ya vyandarua katika kata zake zote 23 na vijiji vyote 111 vya wilaya hiyo ikiwa ni jitihada za kukabiliana na ugonjwa hatari wa malaria.
Mpango huu unakuja baada ya kugundua kuwa baadhi ya wananchi hasa wale waishio mwambao mwa ziwa Tanganyika kuanza kutumia vyandarua kuvulia samaki na kufugia kuku, matumizi ambayo yanakwenda kinyume na malengo ya Serikali ya kupambana na kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini kote
Afisa afya wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Richard Manuma ametembelea vijiji vyote vya wilaya hiyo na kudai kuwa katika kipindi hiki ambacho wameanza zoezi la kuandikisha majina kwenye kaya kwa lengo la kugawa vyandarua, elimu ya matumizi na umuhimu wake itatangulia na baada ya zoezi hilo kila kaya itapewa vyandarua viwili.
Alisema katika vijiji vya Kilewani na Kasanga mwambao mwa ziwa Tanganyika, wakazi wa vijiji hivyo wamekua wakitumia vyandarua kuvulia samaki huku wengine wakifugia kuku na wakati huo wengi wao wakiendelea kushambuliwa na ugonjwa wa Malaria unao sababishwa na vijidudu vya prasmodiamu na kuenezwa na mbu jike aitwaye Anofelesi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.