Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Kalambo Mkoani Rukwa Ndg.Shafi Mpenda amewataka wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi Wilayani humo kuzingatia nidhamu na uadilifu ikiwa ni pamoja na kujiepusha na ulevi wakati wa zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa linalotarajiwa kufanyika Novemba 27/2024.
Ameyasema hayo wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa vituo vya kupigia kura Wilayani humo na kusisitiza wasimamizi hao kuzingatia nidhamu ikiwemo kufungua vituo vya kupigia kura kwa wakati sambamba na kujiepusha na uchukuaji wa video na picha kwenye nyaraka za Serikali.
Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani humo Bi. Lupakisyo Mwakyolile ametumia fursa hiyo kuwataka wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kuzingatia miongozo iliotolewa na Serikali ikiwemo kulifanya zoezi hilo kwa uaminifu na kwa uadilifu sambasambana kujiepusha na vitendo vya Rushwa kwa lengo la kupata viongozi bora na wenye tija katika jamii na taifa kwa ujumla.
Awali akiongea na wasimamizi hao Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la Polisi Wilayani humo SSP Francis Mboya ,amesema jeshi la polisi limejipanga vizuri ili kuimalisha ulinzi na usalama wakati wa zoezi hilo na kusisitiza wasimamizi kutoa taarifa za uharifu na waharifu wakati wa zoezi hilo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.