Wananchi katika vijiji vya mpanga na Mombo tarafa ya mambwenkoswe wilayani kalambo mkoani Rukwa wameiomba serikali kuwapatia misaada ya kibinadamu kutokana na nyumba zao zipatazo 20 kubomoka kutokana na mvua kubwa iliokuwa imeambatana na upepo mkali kunyesha na kubasababisha baadhi yao kukosa makazi na kujihifadhi kwa majirani.
Wananchi hao kwa nyakati tofauti wamesema mvua hiyo imeharibu makazi yao kwa kuezua mapaa na kubomoa nyumba na kueleza kuwa mvua hiyo ilinyesha ikiwa imeambatana na upepo mkali.
Wamesema kufuatia hali hiyo walitoa taarifa kweye uongozi wa kijiji na kata ambao ulifikika eneo la tukio kisha kutoa taarifa wilayani ambao ulifika na kutembelea maeneo yote yaliokuwa yameathirika.
Afisa tarafa ya Mambwenkoswe Mpapalika Mfaume, amekili kuwepo kwa adha hiyo na kusema mvua hiyo ilinyesha na kubomoa nyumba (8) katika kijiji cha Mombo kata ya Legezamwendo na yumba(12) katika kijiji cha Mpanga na kusema mpaka sasa wanaendelea na jitihada za kuwasaidia wananchi waliokumbwa na kadhia hiyo kwa kuwapatia misaada ya kibinadamu pamoja na kusaidia kuzinyenyua nyumba zilizokuwa zimeathirika na kadhia hiyo.
Amesema wameomba sementi kupitia mfuko wa jimbo ili kusaidia ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mpanga ambayo imeezuliwa kutokana na mvua hiyo na kusema sehemu zilizo athirika kwa kiasi kikubwa ni nyumba za wananchi , Kanisa na Zahanati moja.
Kwa upande wake katibu tawala wilayani humo Frank Sichalwe ametumia fulsa hiyo kuwataka wananchi maeneo hayo kujenga mazoea ya kujenga nyumba zao kwa kutumia sementi kwa lengo la kuepukana na adha hiyo
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.