Zikiwa zimesalia siku chache kuelekekea uchaguzi wa serikali za mitaa hapa nchini ,watendaji wa serikali za vijiji na kata zinazopakana na nchi jilani ya Zambia wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kuwa makini na kuhakikisha wahamiaji wote wanaoingia nchini kinyemela na kuanzisha makazi hawashiriki zoezi hilo.
Kumekwepo na changamoto ya baadhi ya raia kutoka nchi jirani ya Zambia kuingia nchini kinyemela na kuchukua kadi za kupigia kura na kuzitumia katika mambo mbalimbali ikiwemo kupiga kura na kujitambulisha kuwa ni watanzania.
Kwa kulitambua hilo katibu tawala wilayani Kalambo Frank Schalwe amekaa kikao na watumishi wa umma kilichoketi katika tarafa ya Mambwenkoswe wilayani humo,amesema zaidi ya wananchi elfu themanini na tisa wamejitindikisha kwenye daftari la wapiga kura hivyo wanapaswa kuhamasishwa ili waweze kuwachagua viongozi wanaowataka.
‘’kazi yetu sisi watumishi ni kuhamasisha watu wote kujitokeza kupiga kura, tunataka tuone watu wote waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wanapiga kura‘’alisema sichalwe.
Kwa upande wake afisa tarafa ya Mambwenkoswe ,Mpapalika Mfaume amewataka watumishi wote kuwa makini na watu wote wanaoishi mpakani kwani waliowengi ni raia wa Zambia.
‘tunahitaji kuona watu wanachagua viongozi wanaowataka na ambao watakuwa msaada kwao na taifa kwa ujumla’’alisema mfaume.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.