Watumishi wa umma wilayani kalambo mkoani Rukwa wamelalamikia kitendo cha wafanyakazi wa serikali waliomasomoni kuto pandishwa madaraja licha ya kufuata vigezo na masharti ya utumishi wa umma wakati wa kwenda masomoni na kuutaka uongozi wa halmashauri hiyo kutoa ufafanuzi zaidi juu ya swala hilo kwa lengo la kuondokanana sitofahamu hiyo.
Wilaya ya kalambo kwa mwaka 2019/2020 imefanikiwa kupandisha madaraja watumishi wapatao 540 huku walimu wakiwa ni 455 na idara zingine ikiwa ni 85 na huku watumishi wapatao 52 wakibadilishiwa miundo yao ya kiutumishi.
Wakiongea kupitia kikao kazi kilichojumuisha watumishi wote wa wauma wilayani humo,wamesema kumekwepo na changamoto ya watumishi waliomasomoni kutopandishwa madaraja licha ya kwenda kwa kufuata vigezo vyote.
Dosephu Ndalama mwenyekiti wa chama cha walimu wilayani humo, amesema wamekuwa wakipata malalamiko kutoka kwa watumishi husani walimu ambao wamekuwa wakienda masomoni bila kupandishwa madaraja.
‘’utakuta mwalimu huyu alipokuwa anaenda masomoni alifuata taratibu zote lakini inakuja kushangaza pale wengine wanapopandishwa madaraja lakini wao wamekuwa wakishindwa kupandishwa sasa hili tuanaona sio haki hivyo tungependa kupata ufafanuzi zaidi kuwa kwanini walimu hawa wapati nafasi’’alisema ndalama.
Aidha aliipongeza serikali kwa jitihada zinazofanywa na serikali ya wilaya hiyo hususani za kupandisha madaraja walimu pamoja na watumishi wengine wote kwa ujumla.
‘’tunamkupongeza sana mkurugezi kwa kupandisha madaraja watumnishi na mpaka sasa kuptia ofisi ya utumishi tumeambiwa kuwa watumishi wameanza kuchukua barua zao za kupandishwa madaraja kwa hilo tunakupongeza sana.’’alisema Ndalama.
Afisa utumishi wilayani humo Amandus Mtani amesema wamepata muongozo mpya kutoka serikalini unaolezea watumishi waliomasomoni kwa muda mrefu kuto pandindishwa madaraja.
‘’kuna muongozo mpya tumepewa serikali ambao unaelezea watumishi waliomasomoni kwa muda mrefu kuto pandishwa madaraja’’alisema Mtani.
Mkurugenzi mtendaji wa hlmashauri ya Wilaya ya hiyo Msongela Mpalela, amewataka watumishi wote kujenga mazoea ya kuchukuliana katika vituo vyao vya kazi kwa kuishi kwa amani bila migogoro kujitokeza.
‘’niwatake watumishi wangu jifunzeni kuchukulina hasa watumishi miliko huko ngazi za chin kwani mkifanya hivyo mtasiwisha upendo na amani kwenye maeneo yenu ya kazi pia lazima mkumbuke kuwa si kila siku ni jumapili kiongozi wako anaweza kukukasirisha kutokana na matatizo ya kifamilia hivyo jifunzeni kuchukulina’’.alisema Msongera.
Katibu tawala wilayani humo Frank Sichalwe amewataka watumishi kuacha tabia ya kuruka ngazi hususani wakati wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao kutoka kwa viongzi husika..
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.