Wavuvi wanaozunguka ziwa Tanganyika kupitia vijiji vya kata ya Kasanga na Samazi wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameipongeza serikali kwa kutoa fedha na kuanza ujenzi wa soko jipya la samaki na kwamba kukamilika kwake litawaondolea adha ya kuuza samaki katika nchi jirani ya Zambia.
Wakiongea katika nyakati tofauti wakati wa shughuli za uvuvi, wamesema kukamilika kwa soko hilo kutawawezesha kuuza samaki zao kwa urahisi zaidi na kwamba itawapunguzia gharama na usumbufu wa kupeleka samaki katika nchi jirani ya Zambia.
‘’tunaipongeza sana serikali kwa kutoa fedha billion 1.4 kwa ajili ya ujenzi wa soko hili kwani uwepo wa soko hili utatusaidia kama wavuvi kuuza samaki zetu katika soko letu badala ya kupeleka Zambia na Kongo ambako wakati mwingine tumekuwa tukipata usumbufu mwingi.’’ Alisema Ahmed Fresh mvuvi.
Hivi karibuni akiongea mara baada ya kutembelea ujenzi wa soko hilo mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kalambo Shaf Mpenda, alisema soko hilo limefikia asilimia 65 ya ujenzi na kwamba ujenzi wa soko hilo umekuja baada ya soko la awali kuzingirwa na maji mwaka 2021 kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Hata hivyo Halmshauri ya Kalambo imenunua boti 2 za kisasa kwa ajili ya shughuli za dolia kwenye ziwa Tanganyika kupitia kata za Kasanga na Samazi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.