Watu wawili kutoka Halmashauri ya Kalambo akiwemo James Chiwalanje Siame mkulima na Beda Lusakas Chipamba mfugaji wameibuka washindi kwenye maonesho ya Nane nene ambayo yalikuwa yakiendelea kufanyika kimataifa jijini Mbeya.
Maonesho ya nane nane kwa mwaka 2023 yamefanyika katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya. Katika maonesho hayo washiriki 574 wakijumuisha kutoka wizara,Taasisi za Umma na binafsi , Asasi za Kiraia ,Wabia wa maendeleo ,Makampuni,Taasisi za Kifedha ,Wakulima,Wafugaji na wavuvi wakiripotiwa kushiriki kwenye maonesho hayo huku watu wapatao laki tano (500000) wakikadiriwa kushiriki kwenye maonesho hayo.
Hata hivyo maonesho ya sherehe za Nane nane hupambwa na ushindanishaji wa wadau wa sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na ushirika na washindi hupewa zawadi mbalimbali kwa kuzingatia muongozo wa mwaka 2017 uliotolewa na wizara ya kilimo ambao unaainisha vigezo vya ushindi ambapo Halmashauri ya kalambo ni miongoni mwa Halmashauri zilizo shiriki kwenye maonesho hayo kwa kushindanisha watu kadhaa ambapo kati yao ni James Chiwalanje Siame ambae amepata zawadi ya fedha million nne na Beda Chipamba akipata zawadi ya fedhga shilling million nane 8,000,000/=.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.