Wananchi Mkoani Rukwa Wameshauriwa kutatua migogoro Kwa Njia ya ustaarabu,amani , mazungumzo na Upatanishi ili kurudisha Mahusiano ya Kirafiki ambayo yatasaidia Katika Upatikanaji wa haki bila kufungwa na masharti ya kisheria ukilinganisha na njia ya uendeshaji wa Mashauri kwa njia ya mahakama ambayo imekuwa ikichukua Muda Mrefu
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Tano Mwela Januari 22/2023 wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria ambayo kwa ngazi ya wilaya yamefanyika kwa kufanya matembezi kutoka eneo la Santamaria hadi katika ofisi za Mahakama ya wilaya hiyo
Amesema utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi ni takwa la katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ,ambapo utekelezaji wake ni muhimu ili kuendana na kasi ya shughuli za ukuaji wa uchumi wa wananchi
‘’hivyo njia mbadala ya utatuzi wa migogoro inajumuisha utaratibu wa usuluhishi ,upatanishi,kurudisha mahusiano ya kirafiki na mazungumzo kufikia makubaliano ‘’ alisema Mwela
Alisema licha ya hilo mahakama inawajibu wa kuongoza waadawa katika kufikia makubaliano ,kuandaa wataalamu wa usuluhishi ikiwemo majaji na mahakimu kwa kuwaongezea ujuzi kwa njia ya mafunzo ,pamoja na kuweka mazingira rafiki ya usuluhishi na kutoa elimu kwa umma
Mapema akiongea na hadhara ya wananchi katuka maeneo hayo hakimu mfawidhi mkazi wa mahakama ya wilaya ya Kalambo, Nikison Tem , amesema utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi una faida nyingi ikiwemo upatikanaji haki kwa wakati na kwa gharama nafuu
Hata hivyo maadhimisho ya uzinduzi wa wiki ya sheria unafanyika katika maeneo mbalimbali ambapo kwa ngazi ya kanda umefanyika katika mahakama kuu kanda ya sumbawanga mkoani Rukwa na kuzinduliwa na jaji mkuu kanda ya Sumbawanga Dastan Ndunguru,
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.