Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Rukwa imefanikiwa kuokoa jumla ya shilingi 10,880,000/= kutoka kwa wadaiwa sugu ambao ni watendaji wa vijiji vya Kizombwe, Kalembe na Mkowe wilayani Kalambo baada ya kufanya ukaguzi kwenye maeneo ya Halmashauri hiyo.
Kaimu mkuu wa Takukuru mkoani Rukwa Daniel Ntepa, alisema lengo ni kuhakikisha wadaiwa sugu wote wanarejesha fedha za serikali na kusema.
‘’Katika kipindi cha mwezi januari hadi Machi 2020 ,tulifanikiwa kuokoa jumla ya fedha tsh 10,880,000 kutoka kwa wadaiwa sugu ambao ni watendaji wakusanyao mapato kwa njia ya POS katika Halmashauri ya Kalambo, ambapo kijiji cha Kizombwe tumeokoa tsh 520,000/=,kijiji cha Kalembe tumeokoa tsh 3,100,000/=, kijiji cha Sopa tumeokoa tsh 4,460,000/= na kijiji cha Mkowe tumeokoa tsh 2,700,000/=’’ .
Hata hivyo katika hatua nyingine taasisi hiyo imefanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya lami yenye umbali wa kilometa 2 kijiji cha Matai wilaya ya Kalambo uliyokuwa unatekelezwa na mkandarasi wa kampuni ya Grand tech Limited ya Dar es salaam baada ya kuingia mkataba na mratibu wa (TARURA)
‘’tarehe 4/3/2019 kwa- gharama ya tsh .899,755,000/=, mkandasi alipaswa kuanza kazi hiyo tarehe 19,3,2019, na kukamilisha kazi ndani ya kipindi cha mkataba na aliomba muda wa nyongeza, ambapo alipewa muda mpaka tarehe 2,11,2019 ili amalize kazi, lakini hata ulipofika muda huo wa nyongeza mkandarasi alikuwa hajamaliza kazi na kuikabidhi kwa mwajiri wake (TARURA) wilaya ya Kalambo’’
Alisema kupitia maombi ya malipo hayo ya tsh 121,584,828.44/= ya mkandasi katika interin payment certificate No 05, mwajiri (TARURA) alimkata mkandarasi liquidated daimage ya tsh 53,985,300/=, kati ya fedha hizo alizoomba kwa usimamizi wa TAKUKURU ambayo ni makato ya kuanzia tarehe 1/11/2019 hadi 1/1/2020 ambayo ni sawa na 0.1% ya gharama za mradi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.