Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amewagiza viongozi wote wa Halmashauri pamoja na wakuu wa wilaya mkoani humo kusimamia kwa ukaribu zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na kuahakikisha kila mwananchi anashiriki na kujiorozesha kwenye daftari hilo.
Akiwa katika ziara ya ukaguzi wa vituo vya kuandikisha wapiga kura wilayani Kalambo ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika 24 Novemba 2019, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo, amesema mapaka sasa wananchi lakimbili hamsini na tisa elfu mia saba themanini na tatu wamejiandikisha na huku wilaya ya Kalambo wakijiandikisha kwa asilimia 36.
‘’ lakini niwatake wakuu wa wilaya pamoja na viongozi wengine zoezi hili linatoa taswira jinsi ya uchaguzi wa mwakani utakavyokuwa’’amesisitiza Wangabo.
‘’ jumla ya wananchi 259,783 mkoani Rukwa wameandikishwa, ambapo wilaya ya Kalambo wananchi wameandikishwa kwa asilimia 36,Nkansi 35,Manispaa ya Sumbawanga asilimia 37 na Hamlamshauri ya Sumbawanga ikiwa ni asilimia70 na kufanya jumla kuwa ni asimilia 45.7 mpaka sasa’’amesisitiza Wangabo.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura, amesema Mawakala wa vyama vya siasa wanalojukumu la kuwasaidia wandikishaji kuwatambua wageni ili wasijiandikishe kwenye daftali la wapiga kura kwani hawana haki hiyo kisheria.
‘’niwatake wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili tuweze kupiga kura ifikapo November 24,2019.Pia watumishi wote wa serikali mnatakiwa kujiandikisha’’alisisitiza Binyura.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.