Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa Dkt. Lazaro Komba amewataka Wananchi kujenga utamaduni wa kufanya utalii wa ndani ili kujifunza na kujionea mandhari yenye vivutio mbalimbali vilivyopo Wilayani humo ikiwemo maanguko ya maji ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika kwa mita 235.
Ameyasema hayo wakati akikagua maandalizi ya Tamasha la Utalii lililopewa jina la KALAMBO FOREST UTALII FESTIVAL ambapo kwa ngazi ya Mkoa Tamasha hilo litafanyika tarehe 14/2/2026 katika eneo ya maanguko ya maji ya Mto Kalambo na kuongeza kuwa Tamasha hilo litaenda sambasamba na michezo ya riadha ikiwemo kukimbia mbio ndefu na fupi kuanzia km 2 hadi km 15 lengo likiwa ni kuimarisha viungo vya mwili na kudumisha umoja, mshikamano na utamaduni wa Wananchi wote.
Hata hivyo, amebainisha kuwa Tamasha hilo litaenda sambamba na mashindano ya ngoma na kuvitaka vikundi mbalimbali vya ngoma kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye mashindano hayo kwani yatahusisha utolewaji wa zawadi mbalimbali ikiwemo medani maalumu.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TFS Wilayani humo ndugu Chesko Lunyungu,amesema maandalizi ya Tamasha hilo yamekamilika vizuri na kuwataka Wananchi na Watumishi wa Umma kujitokeza kwa wingi kushiriki mashindano hayo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.