Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imefanikiwa kutoa elimu juu ya utapia mlo mkali kwa wazazi na walezi wapatao 57000 katika vijiji 111 vya wilaya hiyo kati yao wazazi wenye watoto kati ya miezi 0-6 wakiwa 23784, wazazi wenye watoto kati ya miezi 6-23 wakiwa 12346 na wazazi wenye watoto zaidi ya miezi 23-59 wakiwa 13102 na kufanya jumla ya walengwa 49,232 sawa na asilimia 86.4 walio fikiwa.
Afisa lishe wilayani humo Robart Tepeli kupitia kikao cha lishe robo ya kwanza kwa mwaka 2023/2024 amesema kwa kushirikiana na idara ya kilimo wamefanikiwa kutoa elimu kwa wakulima 990 katika vijiji vya kata ya Ulumi kwa kuhamasisha kulima kilimo cha mboga mboga na matunda sambamba na kuandaa mashamba darasa kwa kila shule.
Awali akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya hiyo Dkt Emanuel Mhanda,akawataka watendaji wa vijiji na kata kulichukulia swala la lishe kwa uzito kwa kuchukua hatua ya kushirikiana na walimu wa shule za msingi na sekondari katika kuhamasisha upatikanaji wa vyakula shuleni.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.