Baraza la wafanyakazi wilayani Kalambo mkoani Rukwa limeishauri serikali kuona uwezekano wa kutoa mafunzo kwa watumishi wa ajira mpya ili kuongeza kasi ya ufanisi wa kazi sambamba na kuwawezesha kukabiliana na mazingira mahali pa kazi.
Mapema akiongea kupitia mkutano wa baraza la wafanyakazi uliokuwa na lengo la kufanya tathimini ya kazi zilizofanyika kwa mwaka 2023, katibu wa chama cha walimu CWT wilayani Kalambo Danstan Mshanga,ameishauri serikali kupitia halmashauri kuweka utaratibu maalmu utakaowezesha watumishi wa ajira mpya wakiwemo walimu kupata mafunzo yatakayo wawezesha kumudu mazingira mahali pa kazi.
Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania CWT mkoani Rukwa Doseph Ndalama ametumia fursa hiyo kuishauri serikali kuweka utaratibu mzuri wa kulipa madai mbalimbali ya watumishi ikiwemo likizo na uhamisho ili kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Hata hivyo mkutano huo ulishirikisha viongozi wa vyama vya wafanyakazi ikiwemo TUGHE, TALGWU na CWT pamoja na wakuu wa idara na vitengo,ambapo kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Nichoraus Mlango aliahidi kutatua changamoto za watumishi ikiwemo kulipa stahiki zao kulingana na miongozo ya serikali.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.