Chama cha mapindizi CCM wilayani Kalambo mkoani Rukwa kimeipongeza ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo kwa kutoa vifaa mbalimbali vya ujezi kwa ajili ya umaliziaji wa maboma pamoja na ukarabati wa majengo ya shule na zahanati .
Ofisi ya mkuu wa wilaya ya kalambo imekuwa na utaratibu wa kutoa misaada kila mwaka kulingana na uhitaji wa maeneo husika,ambapo kwa mwaka huu iilitoa vifaa vya ujezi ikiwemo bati na saruji na kuwakabithi watendaji na madiwani kwa lengo la kusaidia umaliziaji wa majengo kwenye kata na vijiji tofauti vilivyopo wilayani humo.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilayani humo Alfred Mwanga amesema kwa ujumla ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo nimekuwa ikijitahidi kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto za wananchi hususani maeneo ya vijijini.
‘’tunakupongeza kutoa misaada hii,lakini madiwani wapo, watendaji wapo,wenyeviti wa vijiji wapo hivyo sitegemei kuona eti sikumoja unapewa taarifa kuwa misaada ulitoa haikutumika vile inavyotakiwa na wakati wahusika wote wapo itakuwa ni majabu ‘’alisema Mwanga.
Mbali na hayo amelaani vikali kitendo cha baadhi ya viongozi kuto unga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya mungano waTanzania John Paombe Maghufuli nakusema watu hao si wema katika taifa hili.
Mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura amewataka wananchi pamoja na wachungaji kuendelea kumuombea Rais Wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayo ifanya .
Hata hivyo kwa mwaka 2019 ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo imetoa misada ya vifaa vya ujezi kwa mashirika ya dini,watu binafus pamoja na kwenye taasisi ya za serikali vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.