WANANCHI wa kata ya Mambwekenya Wilayani Kalambo wamejikuta katika sintofahamu baada ya kuzuiliwa kushiriki mazishi ya kiongozi wa baraza la machifu mkoani Rukwa ,chifu Christofa Kutazungwa aliyezikwa bila jeneza huku akiwa amekaa kwenye kiti chake na ngozi ya ng’ombe ikilazwa chini badala kumzika mtu mzima kama sadaka.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati mazishi ya chifu huyo wamesema mazishi ya machifu yamekuwa yakifanyika nyakati za usiku tofauti na mazishi hayo ambayo yamefanyika mchana na huku watu wakizuiliwa kulia na kushiriki kuchimba kaburi pamoja na maziko.
John Sichula mkazi Kijiji cha Mambwekenya ,alisema kwake tukio hilo limekuwa la kwanza kuona mtu akizikwa bila jenaza na kusema wamezoa kushiriki katika mazishi ikiwemo kuchimba makaburi lakini imekuwa tofauti kabisa na mazizishi ya chifu huyo.
Alisema licha ya hilo wamezoea kuona mazishi ya machifu yakifanyika nyakati za usiku lakini imekuwa tofauti kwa kiongozi huyo kutokana na kuzikwa muda wa mchana huku kila mtu akiwa anaona na hivyo kuonekana ni kitu kigeni kwao.
Naye Boidi Sichula mkazi wa maeneo hayo ,alisema kilicho mshangaza ni kuona chifu anazikwa akiwa amekaa na ngozi ya ng’ombe kutandikwa chini na kusema katika maisha yake yote hajawahi kuona kitu kama hicho.
Daud Mbaya makazi Wa maeneo hayo,alisema kilicho mshangaza zaidi nikuona watu wakizuiliwa kushiriki mazishi hayo pamoja na kulia wakati wa msiba.
‘’tumezoea akina mama wakilia wakati wa msiba lakini imekuwa tofauti kwa kiongozi huyo kutokana na watu kuzuiliwa kulia zaidi ya kucheza ngoma na kuiomba nyimbo’’alisema .
kwa upande wake kiongozi anaesimika machifu mkoani humo Richad Sinyangwe,alisema wanazika na ngozi ya ng’ombe ikiwa ni badara ya sadaka ya kumtoa mtu.
Alisema kipindi cha nyuma ilikuwa ni lazima kiongozi mkubwa kama huyo kuzikwa na mtu aliye hai lakini badae walikaa na kufanya maboresho na kuanza kutumia ngozi ya mnyama pamoja na damu ya mnyama kama ishara ya sadaka.
Alisema kufanya hivyo kuna onyesha kuwa sadaka inapokelewa na mizimu na kusema hakuna madhara yoyote yanayoweza kutokea .
Kwa upande wake chifu Ntono wa nne wa himaya ya Ulungu Maiko Sikazwe ,alisema chifu huyo amezikwa na ngozi na akiwa amekaa lengo ikiwa ni kudumumisha mila ya kichifu.
Mwakilishi wa mkuu wa mkoa huo, Julieth Binyura ambayepia ni mkuu wa wilaya ya Kalambo,alisemac hifu huyo ndie aliyekuwa kiongozi mkuu wa machifu mkoani humo na kifo chake kimewachia simanzi kubwa kutokana na uadilifu aliokuwa nao enzi za uhai wake.
Aidha aliwataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni ishara ya kumuenzi kiongozi huyo ambaye alikuwa mchapakazi mzuri na kuwa mfano wa kuigwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.