Mkuu wa wilaya ya Kalambo Kalorius Misungwi ametoa siku 14 kwa watumishi wote wanaoishi katika manispaa ya Sumbawanga kuhamia wilayani humo na kusisitiza kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote ambao wataenda kinyume na agizo hilo.
Halmashauri ya Kalambo ilianzishwa Disemba 23 /2012 chini ya kifungu 8 na 9 cha sheria namba 287 ya mwaka 2002 ya mamlaka ya serikali za mitaa.
Hata hivyo tangu kuanzishwa kwa Halmashauri hiyo idadi kubwa ya watumishi wakiwemo wakuu wa idara wamekuwa wakiishi katika manispaa ya Sumbawanga ambako ni zaidi ya umbali wa km 50.
Kwa kuzingatia hilo mkuu wa wilaya hiyo Kalorius misungwi amewataka watumishi hao kuhamia katika maeneo yao ya kazi na kusisitiza kuchukua hatua dhidi ya watumishi ambao watakaidi agizo hilo.
Kwa kuzingatia umuhimu wa agizo hilo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashari ya Kalambo Msongela Nitu Palela amesema ‘’ watumishi wote wanao ishi manispaa ya Sumbawanga na kufanya kazi katika Hamashauri ya Kalambo kwamba wanatakiwa kuhamia Halmashari ya Kalambo ndani ya siku 14. Watumishi wote wa Halmashauri ya Kalambo wanatakiwa kutekeleza agizo hili kwani atakaye puuza agizo hili hatua kali za kinidham zitachukuliwa dhidi yake’’.alisisitiza Msongela.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.