Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imekwama kuendelea na hatua ya robo fainali ya mashindano ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) ambayo kwa ngazi ya kitaifa inafanyika jijini Tanga huku ikishia katika hatua ya 32 bora na mingine ikitolewa katika hatua za awali.
Michezo hiyo inashirikisha Halmashauri 150 nchini ambapo Halmashauri ya wilaya ya Kalambo ni miongoni mwa Halmashauri zilizoshiriki mashindano hayo kwa kushirikisha michezo sita (6) ikiwemo mpira wa Netiball, Ngoma Darts, Karata Bao na Uchoraji huku sababu za kushindwa kuendelea na mashindano hayo Ikitajwa kuwa ni ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani maandalizi hafifu na uzoefu kwa wachezaji kwa baadhi ya michezo.
Hata hivyo michezo hiyo ilizinduliwa na Naibu Waziri ofis ya Rais TAMISEMI DKT. Zainabu Katimba ambae alitumia fursa hiyo kuwaagiza wakurugenzi kuimarisha vitengo vya michezo kwa kuhakikisha kila Halmashauri zinashiriki kikamilifu kwenye mashindano hayo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.