Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Julieth Binyura ametoa siku saba kwa kampuni ya kichina inayotengeneza barabara ya lami kutoka Sumbawanga-Matai-Kasanga mwambao wa ziwaTanganyika kulipa mishahara pamoja na kutoa mikataba kwa wafanyakazi wao na kuahidi kuwaweka ndani viongozi wote wa kampuni hiyo endapo watashindwa kutekeleza agizo hilo.
Kumekwepo na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni ya kichina ya‘’Joint Venture of China Railway 15G and new centry co ltd’’ kutotoa mikataba pamoja kutopeleka fedha kwenye mfuko hifadhi wa taifa wa jamii NSSF licha ya wafanyakazi hao kukatwa fedha na kamapuni hiyo kupitia mishara yao na kumtaka mkuu wa wilaya hiyo kuingilia kati swala hilo.
Awali wakiongea mbele ya mkutano wa hadhara ulifanyika katika kata Kasanga wilayani humo ,wamesema wanahofu na mashaka juu ya kutolipwa sitahiki zao kutokana na mradi huo kutakiwa kukamamilika November 2019 na kuwa kila wakienda NSSF kufuatilia mafao yao wamekuwa wakiambiwa kuwa hakuna fedha zilizoingizwa kwenye acont zao na mwajiri wao.
Wamesema serikali kupitia mkuu wa wilaya haina budi kuingilia kati swala hilo kwa kutoa maagizo kwa wahusika ili waweze kuingiziwa fedha zao kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii.
Jacksoni Mayunga mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo,amesema licha ya hilo wafanyakazi waliowengi kwenye kampuni hiyo hawana mikataba na wengine wamekuwa wakifukuzwa kazi bila kupewa barua hali ambayo imekuwa ikiwapatia ugumu hususani wakati wa kudai mafao yao NSSF.
Meneja wa NSSF mkoani Rukwa Salawa Hangumbalo,amesema endapo fedha zikipelekwa NSSF wafanyakazi wote watalipwa na kuwasihi wafanyakazi hao kufika kwenye ofisi za mfuko huo kutoa taarifa pindi kunapotokea changamotoa yoyote.
mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura amelazimika Kuingilia kati swala hilo na kutoa siku saba kwa kamampuni hiyo kupeleka fedha kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii wa taifa NSSF pamoja na kutoa barua za wafanyakazi wote ambao walikuwa wameachishwa kazi kwa lengo la kuondokana na migogoro isiokuwa ya lazima.
‘’natoa maagizo kwa uongozi wa kampuni hii ,nataka ndani ya siku saba mtoe barua kwa wafanyakazi wote ambao walikuwa wameachishwa kazi pia mtoa mikataba kwa kila mafanya kazi wenu na endapo mkishindwa kufanya hivyo mkurugezi wa kamapuni pamoja na viongozi wengine nitawaweka nadani’’Alisema Binyura.
Mradi wa ujenzi wa barabara ya lami ya Sumbawanga – Matai – Kasanga yenye urefu wa km107 unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania na kugharimu Shilingi Bilioni 133.2 ambapo ujenzi wake unategemewa kumalizika mwezi November 2019 chini ya Mkandarasi Joint Venture of China Railway 15G/New Century Company Ltd.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.