Wananchi Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa wametakiwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa zoezi la upigaji kura ikiwemo kuwahi kwenye vituo vya kupigia kura kwa lengo la kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kuchagua Viongozi wanao wataka kwa maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kalambo ndugu Erasto Mwasanga na kusema vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa moja kamili (1:00) asubuhi hadi saa kumi kamili alasiri na kwamba vituo vilivyopo maeneo ya Magereza na Vyuo vya Ufundi vitafunguliwa saa mbili kamili (2:00) asubuhi na vitafungwa saa tisa kamili (9:00) alasiri.
Aidha, amesema Wasimamizi wa Vituo, Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo, Makarani, waongoaji wapiga kura na walinzi wa vituo watafika eneo la vituo kabla ya saa kumi na mbili (12:00) asubuhi kwa ajili ya maandalizi.
Kwa upande wake Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Ndugu Laurent Kapimpiti ameongeza kuwa watu waliopo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wenye kadi ya mpiga kura ndio watakao ruhusuiwa kupiga kura.
‘’tume inaweza kuruhusu wapiga kura ambao kadi zao zimepotea kupiga kura kwa kutumia utambulisho mwingine. Wapiga kura hao lazima wawe wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura’’. Alisema Kapimpiti.
Baadhi ya Wananchi Wilayani humo wamesema watajitokeza kwa wingi ili kupiga kura kwa lengo la kutimiza haki yao ya kikatiba katika kuwachagua viongozi bora na wanao wataka.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.