Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Dkt.Lazaro Komba amewataka wananchi wilayani humo kupanda miti ya kutosha kuzunguka maeneo yao ya makazi na maeneo ya wazi ili kuepuka adha ya nyumba zao kuezuliwa na upepo.
Ameyasema hayo baada ya kujitokeza kimbunga katika mji mdogo wa Matai halmashauri ya wilaya ya Kalambo kilicho ezua nyumba 22, na watu kadhaa kukosa makazi katika kijiji cha Matai B, ambapo amesisitiza jamii kutunza na kulinda mazingira kwa kupanda miti ya kutosha kwenye maeneo ya makazi ikiwani ni Pamoja na kujenga nyumba bora na imara.
Kwa upande wake Afisa Mazingira wilayani humo Julieth Tarimo amesisitiza umuhimu wa kupanda miti ya vivuli na matunda kwani husaidia kuepusha upepo mkali na kupunguza athari za maafa.
Aidha ametoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupanda miti kwenye vyanzo vya maji (mito,ziwa), na kuzuia ukataji miti kiholela.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.