Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Dkt.Lazaro Komba amewagiza watendaji wa kata wilayani humo kuhakikisha kila shule inakuwa na akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ili kuwezesha wanafunzi kupata chakula muda wote.
Ameyasema hayo kupitia kikao cha kupitia taarifa za utekelezaji wa afua za lishe Robo ya kwanza kuanzia Septemba 2024 na kusisistiza watendaji wa kata kuweka mpango kazi utao wezesheza kila shule kulima mazao kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wakiwa shule badara ya kutegemea michango ya wananchi.
Kwa upande wake afisa lishe wilayani humo Robart Tepeli amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025 halmashauri ilitenga fedha shilingi 81,310,121.61 huku kati ya hizo mapato ya ndani ikiwa ni shilingi 30,000,000.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.