Mkuu wa wilaya ya kalambo mkoani Rukwa Lazaro Komba amezitaka mamlaka zinazo simamia mabaraza ya aridhi ya kata kutoa uelewa sahihi juu ya mipaka ya utendaji kazi zao ili kuepusha mabaraza hayo kusababisha migogoro badala yake ijikite kusuruhisha na kutoa ushauri.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimnisho ya kilele cha wiki ya sheria ambayo kwa ngazi ya wilaya yalifanyika katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa .Ambapo alisema mwaka 2021 serikali ilitoa muiongozo ya mabaraza ya kata kuto toa hukumu na kubaki na jukumu la kushauri lengo ilikuwa kupunguza migogoro ya aridhi.
Hakimu mfawidhi mkazi wa mahakama ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa NicksonTemu amesema serikali imewezesha kupunguza gharama za kufungua mashauri kama vile malipo kwa njia ya mtandao na kurahisha utoaji wa huduma kwa wananchi .
‘’mfumo huu umewezesha kurahisha utoaji huduma kwa wananchi kwani kwa sasa mwananchi anaweza kulipia gharama ,faini na tozo nyingine za mahakama kwa urahisi zaidi kwani kwa sasa hakuna malipo ya aina yoyote yanayo paswa kulipwa kwa pesa tasilimu mahakamani.alisema Tem.
Hata hivyo Mahakama ya wilaya ya Kalambo kwa mwaka 2023 ilifaniiwa kusajili mashauri 146 na kufanikiwa kumaliza mashauri 160 huku mahakama za mwazo zikifanikiwa kusajili mashauri 442 na kumaliza mashauri 447.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.