*UMUHIMU WA KUFANYA MAZOEZI KATIKA MAISHA YAKO.
Leo nizungumzie mambo haya matatu niliyoanza nayo hapo juu.Kwa wale ambao wanafanya mazoezi kila siku na wale ambao wanafanya mara mbili au tatu kwa wiki.
Swali :Kwa nini unafanya mazoezi ?
Unafanya mazoezi kwa ajili ya afya bora ili kuepuka maradhi ya mara kwa mara ambayo pia ni rahisi kupata kwa mtu ambaye hafanyi kabisa mazoezi katika maisha yake.
Pia mazoezi yanasaidi kukufanya kuonaekana kijana mchangamfu wakati wote na pia
hukuongozea maisha.
Mazoezi husaidia moyo wako uwe madhubuti katika mapigo yake, kufungua zaidi mishipa ya damu inayopeleka na kutoa damu katika moyo.
Pia mazoezi huwezesha mapafu yako kuwa na uwezo wa kupumua bila kusikia tofauti yoyote wakati wa mazoezi na baada ya mazoezi ukiwa umepumzika.
Magojwa mengine ambayo utaepukana nayo ukiwa unafanya mazoezi ni kama vile kansa, pumu na ugonjwa wa moyo mazoezi ni dawa tosha kwa haya maradhi niliyo kujulisha hivyo usifanye ajizi anza sasa uone faida yake.
Hali kadhalika kwa wale wenye maradhi ya ukimwi mazoezi husaidia sana kurefusha maisha yao.
MAZOEZI UNAYOHITAJIKA KUYAFANYA MUDA WAKE
Yapo mazoezi ya aina nyigi yakiwapo ni pamoja na kuendesha baiskeli, kucheza mpira wa wavu, kutembea kwa mwendo wa haraka au kwenda sehemu maalum ya kufanyia mazoezi (fitness centre) na kuogelea.
Muda wa kufanya mazoezi usipungue dakika 30-60 kwa muda huu utakuwa umefanya mazoezi ya kutosha kwa siku hiyo.
Siku hizi imekuwa ni jambo la muhimu na la maana sana kufanyia mazoezi kwenye sehemu maalum (fitness centre) Huku kunakuwa na wataalam ambao wanasimamia na kufundisha aina ya mazoezi unayotakiwa kufanya yakiwemo madarasa ya aerobics na gym kunyanyua vitu vizito na kujenga mwili.
LEO TUZUNGUMZIE MAZOEZI YA AEROBICS.
Je? unapata nini kwenye aerobics.
Kwa mujibu wa afisa michezo wilayani Kalambo mkoani Rukwa Mosi Mewa anasema kufanya aerobics kila siku inakufanya uwe na uwezo wa kuwa na mapigo mzuri moyo.Hukusaidia mapafukutumia hewa ya oksijen kwa uhakika na pia kudhibiti uzito wa mwili na kukufanya uwe mchangamfu kila wakati.
NINI MAZOEZI YA AEROBICS
Aerobics maana yake ni matumizi hisika ya oksijen katika mazoezi ya viungo ambayo yanaongozwa na muziki maalum kwa ajili ya mazoezi ya mwili.
Mazoezi ya aerobics yanasaidia kufanya moyo uwe uwezo madhubuti wa kusukuma damu kutoka kwenye moyo na kwenda mwilini na kurudi tena kwa mzunguko wa kawaida bila kuwa na dosari.
Mazoezi ya aerobics yanakufanya kupumzisha akili kwa kupunguza mawazo maana ukimaliza kufanya haya mazoezi hujisikia kupumzika.
Halikadhalika huondoa maumivu ya misuli yako ya mwili na huongeza uwezo wako kimwili kukufaya mtu mwenye furaha wakati wote.
MAZOEZI YA AEROBICS NI KWA AJILI YA NINI?
Mazoezi ya aerobics ni kwa ajili kila mtu bila kujali jiinsia au umri hii ni kwa ajili ya watu wote ambao wameamua kufanya mazoezi ya mwili kwa ajili ya afya zao.
Baada ya utafiti wangu wa takriban miaka kumi katika mazoezi ya aerobics, darasa la aerobics lilikuwa likihudhuriwa na idadi kubwa ya wanawake kuliko wanaume hii ilikuwa ni fikra potofu walizokuwa nazo wanaume kwamba mazoezi ya aerobics ni kwa ajili ya wanawake tu.
Lakini kuanzia mwaka wa 2000 kumekuwa na mabadiliko kwa wanaume wengi kujiunga na mzoezi ya aerobics hivi sasa kuna mwamko mkubwa kwa wanaume kufanya haya mazoezi. Katika kufanya mazoezi aerobics inaupa mwili uwezo wa kupitisha hewa ya oksijen kwa urahisi zaidi na uhakika na pia kuupa moya uwezo wa kupiga mapigo yake kwa dakika wakati unapofanya mazoezi.
Mazoezi ya aerobics ni lazima yafanyike japo kwa muda wa dakika 30-60 na iwe ni mara 3 au 5 kwa wiki kwa ajili ya kuufanya mwili kuwa mchangamfu kwa wakati wote na kupunguza mafuta na uzito uliokithiri.
MAZOEZI YA AEROBICS NA MOYO
Hewa ya oksijen ni muhimu sana mwilini kwa ajili ya kuruhusu kemikali kupelekwa kwenye mwili.
Moyo umetengenezwa kwa misuli ambayo husukuma hewa ya oksijen na damu kwenye mwili wote.
Mazoezi ya aerobics huzidisha uwezo wa mapafu kuyapa oksijen na kuipa nguvu misuli ya moyo na kuwa na uhakika wa kuaminika kwa kusukuma oksijen na pia husaidia kuondoa maradhi ya moyo.
Binadamu wa kawaida ambaye hafanyi mazoezi mapigo yake ya moyo ni mara 75 kwa dakika lakini kwa wale wafanyao mazoezi kila siku mapigo ya moyo wao huwa mara 55 kwa dakika.
MAZOEZI YA AEROBICS YANAVYOSAIDIA KUTOONGEZEKA UZITO WA MWILI
kwa mijibu wa mwalimu mratibu wa michezo wilayani Kalambo Baraka Mazengo anabainisha kuwa Mtu huongezeka uzito pindi anapokula bila mpangilio (kula hovyo) kula chakula kwa wingi bila kupanga wakati wa kula na kula milo zaidi ya mitatu bila kufanya mazoezi.
Ni vizuri kupata lishe bora ambayo haina mafuta sana na mazoezi kwa ajili ya kupunguza uzito kwa uhakika zaidi ya mlo wako wa siku pata chai ya kutosha asubuhi mchana pata chakula kama ulikuwa unakula sahani ya chakula iliyojaa kula nusu sahani na usiku pata chakula chepesi kwani nyakati za usiku mwili hauhitaji tena virutubisho vya aina yoyote ile hadi kesho yake.
NAMNA YA KUEPUKA KULA BILA MPANGILIO
Kuna njia nyingi ambazo zitakufanya ubadilishe tabia ya kula bila mpangilio lakini njia bora ya kufuatia ni kuanza kupunguza kula vitu vya sukari polepole na hii ni baada ya wiki kadhaa utakuwa umezoea na hutorudia tena mazoea hayo kumbuka nikizungumzia vitu vya sukari ni kama vile chocolate,soda,keki Unaweza kula vitu kama matunda ambayo yana sukari ya kutosha.
Pia jaribu kuepuka kula nyama nyekundu nikiwa na maana nyama ya ng’ombe na mbuzi, bali utumie nyama ya kuku na samakiKumbuka unavyofanya mazoezi ndio utakavyokula vizuri bila kuogopa utaongezeka uzito
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.