Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imepanga kukusanya na kutumia Kiasi cha shilingi 34,060,221,000.00 kama bajeti kuu ya mwaka wa fedha 2024/2025 huku kiasi cha shilingi 2,412,405,00 kikitarajiwa kutoka kwenye mapato ya ndani.
Akiongea kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo ,afisa mipango na uratibu wilayani humo Erasto mwasanga,amesema katika kufanikisha utekelezaji wa bajeti hiyo vyanzo vipya vya mapato vimeongezwa ikiwa ni pamoja na mapato yatokanayo na kodi ya Ardhi ,kodi ya majengo na kodi ya mabango na kusema licha ya hilo bajeti imezingatia malipo ya stahiki za watumishi.
‘’ikumbukwe kuwa ukomo uliotumika katika uandaaji wa bajeti hii ni wa mwaka 2023/2024 hivyo basi mabadiliko yatakuwepo hasa kwa fedha tunazozipata kutoka serikali kuu, pamoja na wahisani pindi watakapotoa ukomo wa hali ya bajeti kwa mwaka 2024/2025.’’alisema Mwasenga.
Alisema licha ya hilo bajeti hiyo imezingatia maslahi ya watumishi ambapo halmashauri imetenga fedha million 41,760,000.00 kama fedha za kujikimu kwa walimu wapya na shilingi 124,460,000.00 zimetengwa kwa ajili ya likizo za walimu na shilingi 87,601,000.000 zimetengwa kwa ajili ya uhamisho wa walimu.
Hata hivyo baraza la wafanyakazi limefanyika kwenye ukumbi wa ofisi za mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa likiwa na lengo la kujadili mapendekezo ya mpango kazi wa bajeti ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.