Mkoa wa Rukwa umepokea msaada wa vifaa vya kutunzia takwimu za huduma za mama na matoto vyenye thamani ya shilingi million kumi na tano na kufadhiliwa na mradi wa uzazi salama na kusambazwa katika vituo vya afya na hosptari za wilaya lengo likiwa ni kuondokana na adha ya kupotea kwa takwimu hizo.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa waganga wakuu wa wilaya na mkoa ,mkurugenzi wa uzazi salama mkoani Rukwa Esteria Kisoka, amesema lengo ni kuhakikisha takwimu hazipotei.
Alisema vifaa hivyo vitagawanywa katika wilaya zote za mkoa huo kupitia kwenye hosptari za wilaya pamoja na vituo vya afya na kusema lengo ni kuhakikisha upotevu wa takwimu unakwisha.
‘’ni imani yetu kuwa vifaa hivi vitaenda kwenye maeneo husika na kufanya kazi ile iliokusudiwa.alisema Kisoka
Kaimu mganga mkuu mkoani humo Dr.Emanuel Mtika, aliupongeza uongozi kutoka mradi wa uzazi salama kwa kutoa msaada huo na kuwa msaada huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa ikiwemo kuondokana na adha ya upotevu wa takwimu.
‘’takwimu ndio kila kitu kwani bila tawikwimu hususani katika miaka ya hivi sasa huwezi kufanya kitu bila takwimu , niwapongeze wenzetu wa uzazi salama kwa kutoa vifaa hivi ‘’alisema Mtika.
Vifaa hivyo vimegawanywa katika Halmashauri za Kalambo, Nkasi , manispaa ya Sumbawanga pamoja na Halmashauri ya Sumbawanga na huku lengo kubwa ikiwa ni kusaidia kuondokana na adha ya upotevu wa takwimu haswa za mama na mtoto.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.