Serikali kupitia miradi yake ya Afya na Usafi wa Mazingira(SWASH) Pamoja na mradi wa Lipa kulingana na Matokeo (EP4R) imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa jumla ya kiasi cha Shilingi 1,152,557,008.77/= kwaajili ya kutekeleza ujenzi wa madarasa 18, matundu ya vyoo 178, mabweni mawili kwa shule za Msingi na Sekondari.
Mbali na fedha za miradi hiyo wananchi wa Kata ya Matai kwa kushirikiana na halmshauri wameanza ujenzi wa vyumba vya madarasa manne katika shule ya Sekondari Matai ambavyo vinatakiwa kukamilika kabla ya tarehe 28.2.2021 kwaajili ya kuwapokea wanafunzi 254 waliokosa nafasi katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wa wananfunzi hao wilayani humo.
Akizungumza katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya shule za Msingi za Sekondari katika Halmshauri hiyo mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo wakati alipokuwa katika Shule ya Sekondari Matai inayotekeleza ujenzi wa madarasa saba na mabweni mawili, amesema miradi hiyo inatakiwa kukamilika haraka ili kuwawezesha wanafunzi waliokosa nafasi kuweza kuendelea na masomo.
Wakati akitoa taarifa ya Wilaya hiyo Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Carolius Misungwi alieleza mikakati mbalimbali iliyowekwa na Wilaya ili kufanikisha azima ya serikali katika kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa madarasa hayo na wanafunzi hao kuendelea na masomo ifikapo mwezi Februari 2021.
“Wilaya imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari za Kalambo, Matai, Msanzi, Mwazye na Mambwe. Vyumba sita vya madarasa vya Shule ya Sekondari Wasichana matai vitatumika kwa muda wakati ujenzi wa vyumba 7 unakamilika katika shule ya Sekondari Matai,” Alisema.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.