Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imefanikiwa kusajili kaya elfu arobaini na tatu mia tisa arobaini na nne (43944) tangu kuanza kwa zoezi la Sensa na makazi Agust 23/2022 huku mkuu wa wilaya hiyo Tano Mwela akiwataka makarani kuongeza kasi ya zoezi hilo kwa kuwafikia wananchi wote kabla ya muda uliopangwa na serikali kuisha.
Akiongea Ofisini kwake mkuu wa wilaya hiyo Tano Mwela Aliwataka makarani kuongeza kasi ya zoezi hilo kwa kuchukua taarifa sahihi na kufanya kazi kwa weredi.
Alisema licha ya hilo serikali ilitoa power benk na kuwakababidhi makarani wote kwa lengo la kuviwezesha vishikwambi vyao kuwa na chaji muda wote.
‘’ Mpaka sasa hivi tumesajili kaya 43,944 hivyo nitoe rai kwa wale wote ambao hawajafikiwa kuwa watahesabiwa,kikubwa wajiandae na kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa makarani pindi watakapowafikia kwenye maeneo yao’’Alisema Mwela ‘’
Awali akiongea wakati wa zoezi hilo mratibu wa Sensa na makazi wilayani humo Mjanaeli Swalehe aliwahakikishia wananchi kuhesabiwa kabla ya muda uliopangwa na serikali.
‘’Tuna hakika zoezi hili litakwisha kabla ya muda uliopangwa na serikali, kwani baadhi ya kata tayari zoezi limekamilika na kinachofanyika kwa sasa ni kuwahamishia makarani wote waliomaliza kwenye maeneo yao ili wasaidie kuongeza nguvu katika maeneo yaliyosalia. ‘’Alisema Mjanaeli.’’
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.