Jeshi la polisi mkoani Rukwa limeanzisha utaratibu maalumu wa kuwatambua watumaji wa barabara kwa kutoa mafunzo na kuwatunuku vyeti watumiaji wa vyombo vyote ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali zembe na makosa ya barabarani ambayo yamekuwa yakijitokeza na kugharimu maisha ya watu.
Akiongea wakati wa kufunga mafunzo ya usalama barabarani yaliojumuisha madereva kutoka wilaya tatu za mkoa wa Rukwa ,Kamanda wa jeshila la polisi mkoani humo ACP Wiliam Mwampagale, alisema ajali zimekuwa chanzo cha madhara ya kifamilia ,kijamii na kitaifa na kubainisha kuwa watu wengi wamekuwa wakipata ulemavu wa kudumu na watoto kuachwa yatima kutokana na awepo wa ajali.
‘’zigatieni sheria kanuni na alama za barabarani ilikupunguza ajali zembe (zingatieni utii wa sheria bila shuruti) ‘’alisema Mwampagale.’’
Aidha aliwasisistiza madereva wa magari kuhakikisha wanakagua vyombo vyao mara kwa mara kwa kufunga mikanda wawapo kwenye vyombo vyao na kusistiza kutoendesha vyo vya moto kwa mazoea.
Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya shule ya usalama barabarani (GACIOUS DRIVING SCHOOL.GDS TANZANIA. Alisema changamoto za uwepo wa ajari zimekuwa zikisababisha watoto kuachwa yatima kutokana na wazazi au walezi kufariki kwa ajali.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.