Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa katika msimu wa mwaka 2023/2024 inatarajia kulima hekta 157,232 za mashamba na kuzalisha tani 388,056 za mazao ya nafaka kati ya hizo mahindi ikiwa ni tani 233, 568, Maharagwe 56,688, Mpunga 10,999, Mtama 115, Ulezi 5,936, Muhogo, 29,940, Ndizi 70, na Viazi Vitamu 6,050.
Kwa mujibu wa kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kalambo Nichoraus Mlango, amebainisha kuwa licha hilo halmashauri inatarajia kulima tani 350 za Soya, Karanga tani 6,233, Alizeti18,079, Miwa 16764, Kahawa tani 2 ,Nyanya 312,Vitungu 516, Vitungu swaumu 98, Chainize 90, Bamia 12,Karoti 12, Kabichi 90, na mchicha Tani 32.
Licha ya hilo amebainisha kuwa Halmashauri ya Kalambo inategemea kilimo cha mahindi kama zao la biashara na kwamba katika msimu ujao Halmashauri inatarajia kulima hekta 72,990 za zao la mahindi na mpunga hekta 3,659.
Hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ina ukubwa wa hekta 319,300 zinazofaa kwa kilimo. Eneo linalolimwa kwa sasa ni hekta 133,604 sawa na asilimia 42 ya eneo lote linalofaa kwa kilimo. Hekta 4,500 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji, hekta 650 zinatumika kwa umwagiliaji (sawa na 14.4%).
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.