Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imefanikiwa kuongeza bajeti ya utekelezaji wa afua za lishe kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kutoka shilingi million 61, 000,000/= kwa mwaka wa fedha 2023/2024 hadi kufikia shilingi milioni 81,310,215.61.
Katika mwaka wa fedha 2021/2022 serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ilisaini mkataba wa utekelezaji wa afua za lishe na wakuu wa mikoa na wilaya ambao ulikuwa na lengo la kutokomeza utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano na wanawake wanaonyonyesha.
Hata hivyo kwa matokeo ya utafiti wa afya na Demografia ya mwaka 2018 ulionyesha udumavu kuwa katika kiwango cha asilimia 32 kitaifa na katika mkoa ikiwa ni 49.9% ambapo kwa kuliona hilo serikali kupitia wakuu wa wilaya walisaini mikataba na wakurugenzi ili kutenga fedha kwa ajili ya watoto wenye hali ya udumavu.
Licha ya hilo halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imekuwa miongoni mwa halmashauri hapa nchini ambazo zimekuwa zikitekeleza mpango huo kwa kiwango cha juu ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 halmashauri imefanikiwa kutenga fedha million 81,310,2015,.61 kati ya hizo shilingi 30,3000,00 zikitengwa kutoka mapato ya ndani na shilingi 51,310,215.61 ikiwa ni kutoka kwenye OC
Kwa mujibu wa Robert Tepeli ambaye ni afisa Lishe wilayani humo, alisema licha ya hilo halmashauri imefanikiwa kuwafikia watoto wote wenye hali ya utapiamlo na udumavu katika vijiji 111 na kata 23 za wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu katika jamii juu ya umuhimu wa kutumia vyakula bora na vyenye virutubisho.
Alisema pamoja na mambo mengine halmashauri imefanikiwa kuanzisha kamati za wilaya vijiji na kata zinazohusika na maswala ya usimamizi wa lishe ambazo zimekuwa zikisaidia kutoa elimu katika vijiji kupitia siku ya lishe ya vijiji ambayo imekuwa ikifanyika kila baada ya miezi mitatu.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Dkt. Lazaro Komba, alisema licha ya hilo wamefanikiwa kuanzisha mashamba darasa katika kila shule ambayo yamekuwa yakisimamiwa na watendaji wa kata kwa kushirikiana na wakuu wa shule ambayo yamekuwa yakirahisisha upatikanaji wa vyakula mashuleni kwa ajili ya wanafunzi kuanzia madarasa ya awali.
Alisema licha ya hilo utekelezaji wa maswala ya lishe wilayani humo umekuwa ukipimwa kupitia alama kadi lishe na kuonyesha wilaya katika utoaji chakula mashuleni ni asimilia 53.2 na kwamba utekelezaji wa afua hizo umekuwa ukifanywa kwa ushirikiano na idara za afya Kilimo, Maendeleo ya jamii na Elimu sekondari kwa kutenga fedha shilingi elfu moja kwa kila mtoto mwenye udumavu ikiwa ni pamoja na kusaidia kutoa elimu katika jamii.
Licha ya hilo kupitia kikao cha utekelezaji afua za lishe Robo ya kwanza ya Julai hadi sptemba 2024, kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Ramadhani Mabula, aliwataka wasimamizi wa utekelezaji wa mpango wa lishe wilayani humo kuendelea kuweka bidii katika utoaji elimu katika jamii kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za vitongoji na vijiji ikiwa ni pamoja na kuwasimamia wasimamizi wa lishe ngazi ya jamii ngazi WAVI ili kutoa elimu katika jamii juu ya umuhimu wa lishe kwa watoto.
Baadhi ya wanawake wajawazito mkoani humo akiwemo Neema Mwanawima waliipongeza serikali kwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa afua za lishe na kwamba hatua hayo itasaidia kupunguza kiwango cha udumavu na utapiamlo kwa watoto.
Hata hivyo serikali imekuwa ikitumia 2% ya pato la Taifa kila mwaka ambalo ni sawa na Dola za Marekani million 518 kwa ajili ya ununuzi wa matone ya vitamini A na vidonge vya madini Chuma na asidi ya Foliki kwa ajili ya kuongeza damu lengo ikiwa ni kusaidia kupunguza udumavu na utapiamlo kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.