Kamati ya lishe wilayani Kalambo mkoani Rukwa imeazimia wanafunzi wa shule za msingi kupata chakula cha mchana ikiwa ni jitihada za kutokomeza afua za lishe na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Maazimio hayo yamefanyika kupitia kikao maalumu kilichoketi kwenye ofisi za mkuu wa wilaya hiyo na kukubaliana wanafunzi wote kuanza kupata chakula cha mchana na kuwasihi maafisa elimu kufuatilia swala hilo kwa ukaribu zaidi kwa kuhimiza wazazi na walezi kuchangia vyakula shuleni.
Afisa lishe wilayani humo bwana Krispin amesema hali ya udumavu kwa watoto wilayani humo imepungua kwa kiasi kikubwa na kusema wameweka mkakati wa kuwatembelea wazazi na walezi nyumba kwa nyumba kwa lengo la kutoa elimu juu ya kula vyakula bora.
Mkuu wa wilaya hiyo Kalorius Misungwi amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapata chakula cha mchana shuleni ili kuwawezesha watoto wao kuongeza kiwango cha ufaulu.
Hivi karibuni mashirika yasio kuwa yakiserikali ikiwemo ECD yamekuwa mstari wa mbele katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa wananchi kula vyakula bora na vyenye virutubisho.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.