Wajumbe wa kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) mkoani Rukwa, wamepitisha mapendekezo ya kuligawa jimbo la uchaguzi la Kwela katika wilaya ya Sumbawanga kutokana na kuwa na vigezo vyote ikiwemo idadi kubwa ya watu, hali ya kiuchumi na mipaka ya kiutawala.
Kaimu katibu tawala mkoani humo Donald Nssoko kupitia kikao cha kawaida (maalumu) cha kamati ya maendeleo ya mkoa (RCC), amesema walipokea mapendekezo kutoka kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Sumbawanga baada ya kukaa vikao vya maamuzi ikiwemo baraza la madiwani ambavyo vilipendekeza kugawanywa kwa jimbo hilo.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mhe Makongoro Nyerere, amesema mgawanyo huo unahusisha eneo la Ufipa ya juu linaloundwa na tarafa mbili ikiwemo tarafa ya Mpui na Laela lenye kata 14, vijiji 49 na vitongoji 261 ambalo lilipendekezwa kuwa jimbo la Kwela. Kwa upande eneo la ufipa ya chini Bonde la ziwa Rukwa yenye tarafa mbili, kata 13, vijiji 25 na vitongoji 225 lilipendekezwa kuwa jimbo jipya la Mtowisa na kwamba wajumbe wameridhia mapendekezo ya kugawanywa kwa jimbo hilo.
Hata hivyo tangazo lililotolewa na tume ya uchaguzi Februari 26, 2025 lilieleza kuwa vigezo vitakavyo tumika katika kugawanya majimbo ni wastani wa idadi ya watu, ambapo kwa majimbo ya mjini ni watu 600,000 na majimbo ya vijijini nikuanzia wastani wa watu 400,000,huku takwimu zitazotumika ni za sensa ya watu na mkazi ya mwaka 2022. Ambapo jimbo la kwela limekidhi vigezo hivyo kutokana na kuwa na idadi ya watu 494,330, hali nzuri ya kiuchumi na mipaka ya kiutawala,
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.