NAIBU waziri wa wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEM),Josephat Kandege amewaagiza maofisa watendaji wa serikali waliopo kata ya Samazi wilayani Kalambo mkoani Rukwa kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya mafundi wanaodaiwa kukwamisha ujenzi wa kituo cha afya Samazi kilichopo wilayani Kalambo.
Agizo hilo alilitoa mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi na kutembelea eneo ambalo ujenzi wa kituo hicho unafanyika na kupewa taarifa kuwa kuna baadhi ya mafundi wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya kwa kugoma kufanya kazi kwa madai kuwa fedha wanazopata kutokana na malipo ya kazi hiyo ni kidogo.
Naibu waziri huyo,Kandege ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo la Kalambo alisema kuwa tayari wananchi wa jimbo hilo wamekwisha kubaliana kuwa yeyote atakaye kwamisha ujenzi wa kituo hicho cha afya nilazima achukuliwe hatua,ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwani hata sheria zinaruhusu kufanya hivyo.
Alisema kuwa ni vizuri kila mwananchi akashiriki kikamilifu katika ujenzi huo wa kituo cha afya kwani kutatatua changamoto zinazo wakabiri za kutembea umbali mrefu kwaajili ya kutafuta huduma za afya.
Kwaupande wake mhandisi wa Halmashauri hiyo,Daud Sebiga alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho cha afya cha Kata ya Samazi kinatarajiwa kukamilika ndani ya siku 90.
Alisema kuwa mpaka hivi sasa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo imekwisha pokea fedha kiasi cha shilingi milioni 400 kutoka serikali kuu ambazo zitatumika kukamilisha ujenzi ndani ya siku 90 wa majengo matatu ambayo yatatumika katika kituo hicho cha afya.
Naye Juma Kibongwe diwani wa Kata ya Samazi aliishukuru serikali kwaniaba ya wananchi wa kata hiyo kwa kutoa fedha hizo ambapo ujenzi wa kituo hicho cha afya utakapo kuwa umekamilika utawaondolea kero wanazokutana nazo pindi wanapokuwa wagojwa.
Ujenzi wa kituo cha afya Samazi uilitakiwa kunza June 2019 baada ya serikali kutoa shilingi milioni 400 kwaajili ya ujenzi huo,lakini umekuwa ukisua sua kutokana na kuibuka kwa mvutano wa eneo gani kijengwe na kukubalina kujenga katika eneo la zahanati .
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.