Dkt.Karemani Awagiza Wakandarasi Kutoa Ajira Kwa Vijana Wazawa.
Posted on: August 28th, 2019
Waziri wa nishati Dkt. Medadi Karemani amewagiza wakandasi wanaondelea kutekeleza mradi wa usambazaji wa umeme vijijini (REA)wilayani Kalambo mkoani Rukwa kufungua ofisi ndogo katika kila kijiji ambazo zitasadia wananchi kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wakati wa kufanya malipo ya huduma hiyo.
Dkt .karema ameyasema hayo wakati wa ziara yake mkoani Rukwa,ambapo akiwa katika eneo la Myunga wilayani kalambo amefungua mradi wa umeme katika kijiji cha Mkali na kuwataka wakandasi kutoa ajira za kazi kwa vijana wanaotokea kwenye maeneo husika sambamba na kufungua ofisi kwa kila kijiji.
Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kila kijiji kinapata umeme kwa muda muafaka na kwa bei nafuu na kuwasihi wananchi kuendelea kufanya malipo sambamba kusuka umeme kwenye nyumba zao kwa lengo la kuwezesha kufanikisha zoezi hilo kwa haraka.
Mkuu wa wilaya ya kalambo Julith Binyura, amewakikishia wananchi wilayani humo kupatiwa umeme katika vijiji vyote na kuwasihi kuepukana na vishoka ambao wamekuwa wakijitokeza kwenye maeneo mbalimbali kwa madai kuwa ni mafundi.