Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa Kenya itakuwa katika maombolezo ya siku tatu baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Benjamin William Mkapa.
Maombolezo hayo kitaifa yatakuwa kuanzia siku ya Jumatatu mpaka Jumatano.
Bendera nchini humo na ya Afrika Mashariki zitapepea nusu mlingoti kwa siku tatu za maombolezo.
Benjamin Mkapa alikuwa na mchango mkubwa kwa Kenya katika masuala mbalimbali hasa ya kidiplomasia, akiwa mmoja kati ya watu muhimu walioshiriki mchakato wa kupatikana kwa amani nchini Kenya wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya za mwaka 2008
Rais John Pombe Magufuli alitangaza usiku wa kuamkia Ijumaa kupitia runinga ya taifa taarifa za kuaga dunia kwa kiongozi huyo wa awamu ya tatu katika hospitali moja jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Rais Magufuli alisema Bw. Mkapa amekuwa akipokea matibabu katika hospitali moja jiji Dar es Salaam, na kuongeza kuwa maelezo zaidi yatatolewa baadae.
''Mzee Benjamin William Mkapa Rais wa awamu ya tatu amefariki. Amefariki kwenye hospitali mjini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa. Niwaombe watanzania tulipokee hili. Taifa limepata msiba mkubwa. Tuendelee kumuombea Mzee wetu Rais Benjamin William Mkapa ambaye ametangulia mbele ya haki," ametangaza rais Magufuli.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.