Ofisi ya Raisi TAMISEMI kwa kushirikiana na wizara ya afya imeandaa kampeni ya kitaifa ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti wenye umri kuanzia miaka 9 hadi 14 waliopo katika shule za msingi na sekondari ili kuwalinda dhidi ya ugonjwa huo.
Hayo yamebainishwa na afisa afya Wilayani Kalambo Queen Nyahenga kupitia uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi iliyofanyika katika shule ya msingi Matai ‘’B’’ wilayani Kalambo mkoani Rukwa na kubainisha kuwa kampeni hiyo inalenga kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo kwa kuhakikisha walengwa wanapata kinga dhidi ya ugonjwa huo na hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wapya.
Kaimu mkuu wa wilaya ya Kalambo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali ametumia fursa hiyo kuwataka wazazi na walezi kulichukulia zoezi hilo kwa uzito kwa kuwaruhusu watoto wao kupata chanjo kwa manufaa yao ya baadaye na kubainisha kuwa babinti 29,966 wanatarajiwa kufikiwa na zoezi hilo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.