Baraza la madiwani wilayani Kalambo mkoani Rukwa limeazimia maaeneo yote ya taasisis za serikali kupimwa na kutoa hati miliki kwa wahusika ili kuepusha mvutano na migongano ya kimasilahi ambayo imekuwa ukijitokeza kutokana na mtu au watu kuvamia na kujimilikisha maeneo ya serikali kinyemera.
Wakongea kupitia kikao kilichofanyika wilayani humo, madiwani hao wamesema kupimwa kwa maeneo ya taasisi za serikali ikiwemo shule na zahanati kutaondoa mvutano ambao umekuwa ukijitokeza baina ya serikalali za vijiji na wananchi kutokaana na baadhi ya watu wasio waadirifu kuvamia maeneo hayo kinyume na utaratibu.
Aidha wamemwagiza mkurugezni mtendaji wa Halmshauri hiyo Shafi Mpenda kuhakikisha anaweka bajeti ya apimaji maeneo hayo.
Kaimu mwenyekiti wa Halmshauri Fotunats Zozimo,amesema wanampango wakukutana na wataamu wa idara ya aridhi ili kuweka mipango na mkakati wa kupima maeneo yote ya taasisi za serikali kuanzia ngazi za vijiji.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Jeshi Lupembe amaesema serikali inampango wa kuliweka swala hilo kwenye bajeti na kusisitiza tasisi zingine ikiwemo TARULA, TANESCO NA LUWASA kuweka bajeti ya upimaji wa maeneo hayo ili kulifanya swala hilo kuenda kwa haraka.
Hata hivyo Halmshauri ya Kalambo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 imefanikiwa kupima viwanja 190 na kwa mwaka 2021 /2022 inatarajia kupima viwanja 1250.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.