Mahakama ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kwa mwaka 2022 imefanikiwa kusajiri mashauri 216 na kumaliza mashauri 184 huku mashauri 32 yakishindwa kumalizwa kutokana na changamoto mbalimbali
Hakimu mfawidhi mkazi wa Mahakam ya wilaya ya kalambo kupitia kilele cha madhimisho ya siku ya sheria, Nikson Tem, amesema kwa mwaka jana Mahakama zilifanikiwa kusajiri mashauri 375 na kumaliza mashauri 367 na kubakiza mashauri 8 na kwamba idadi hiyo ni pamoja na Mahakama za mwanzo
‘’maadhimisho ya siku ya sheria nchini huambatana na kauli mbiu au maudhui na kwamaka huu kauli mbiu yeu ni umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu ;wajibu wa mahakama na wadau’’ alisema Tem
Alisema kauli mbiu hiyo imebeba ujumbe mahususi kuhusu wajibu wa mahakama na wadau wake katika kutumia njia ya usuruhishi katika kutatua migogoro kwa lengo la kukuza uchumi endelevu
Mapema kiongea kupitia maadhimisho hayo wakili wa serikali Marietha Maguta , aliwakikishia wananchi na wadau wa sheria kuwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali itaendelea kusimamia kwa karibu maelekezo yaliotolewa na kutoa kipaumbele chs kumaliza migogoro kwa njia ya maridhiano
‘’msisitizo wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya mbadara na uikilizwaji wa mashauri kwa njia ya za kimahakama kama ulivyowekewa msingi imara kwenye sheria zetu unahitaji kuwekwa mazingira rafiki ,jambo ambalo pia limekuwa likihimizwa sehemu mbalimbali duniani’’ alisema Malietha
Kwa upande wake Deogratus Sanga , alisema TLC imejiwekea mkakati wa kuanzisha kituo cha cha kimataifa cha usuluhishi wa migogoro kwa kushirikina na wizara ya katiba na sheria ambacho kitaiweka Tanzania katika ramani ya Afrika na dunia kwa kutekeleza dhana ya kutatua migogoro ya kibiashara za kimataifa nay a wawekezaji kwa njia ya suluhu
Hata hivyo, Tanzania ni muhimili ulioanzshwa na katiba ya Jamhuri ya mungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo inatoa mamlaka kwa mahakama kuwa chombo cha kutoa haki kwa wakati na kwa wananachi wote
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.