Mahakama ya wilaya Kalambo mkoa wa Rukwa imemhukumu Esther Mwanisawa, mfipa, miaka 32, mkristo na mkazi wa kijiji cha Katuka wilaya ya Kalambo mkoa wa Rukwa kifungo cha nje mwaka mmoja na kazi ngumu kwa kosa la kumjeruhi mwanae mdogo wa siku tatu kwa kumkata uume wake wote.Mtuhumiwa alishitakiwa kwa Kosa Hilo kinyume na kifungu 222(b) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya mwaka 2019.
Mshitakiwa alitenda Kosa hilo mnamo tarehe 26/12/2019 majira ya saa 02:00 huko katika kijiji cha Katuka wilaya ya Kalambo mkoa wa Rukwa, baada ya kumngoja mganga akiwa amelala akaanza kuchukua wembe na kumkata mtoto huyo kwa kushirikiana na wanaume wawili ambao mpaka Sasa hawajapatikana na bado wanatafutwa na polisi.
Mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi matai na kuandaliwa hati ya mashitaka na kufikishwa mahakamani.
Hata hivyo mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na upande wa mashitaka ukawa na jukumu la kuthibitisha bila shaka tuhuma zinazomkabili mshitakiwa. Ambapo Upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka Mrisho Kimbeho na Ndunda Rajabu Uliandaa mashahahidi , ambapo iliwaita mashahidi Wanne (4) akiwemo mtoto wa kike wa mtuhimiwa wa tukio hilo , Daktari wa kituo cha afya cha Matai, Mama mkubwa wa mhanga, pamoja na mpelelezi wa kesi hiyo na kuthibitisha tukio hilo ambapo mashahidi hao walithibitisha bila shaka.
Akitoa ushahidi wake mtoto wa mtuhimiwa alisema wakati tukio linatokea yeye alikuwa ametoka kukujoa nje, mara waliingia wanaume wawili na kumpa kitu mama yake ambaye hakujua ni kitu gani, Kisha Mama mtu akaanza kumvua nguo mtoto yule mdogo na Kisha kutoa wembe na kumkata mtoto yule uume wake Kisha akawambia wale wanaume kuwa tayari na kutoa pesa Tsh 1000/= na kuwapa Kisha wakatoka nje huku wakimtishia yule mtoto kuwa akisema kwa watu watamchinja na yeye, ndio yule mtoto akamua kutoroka na kukimbilia kwa mama yake mkubwa ambaye ni dada wa mtuhimiwa na ndie alikuwa shahidi namba mbili na kumuelezea yote aliyoyaona na kumfanya yule Mama mkubwa kutoa taarifa kwa viongozi wa Kijiji cha Katuka, ambao wakaja kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kituo cha polisi Matai na huku yule mtoto wakimpeleka kituo cha afya matai kwa ajiri ya matibabu ambapo baadae walimpa rufaa na kumpeleka hospitali kubwa ya rufaa mkoa wa Rukwa ambayo Ipo wilayani Sumbawanga kwa matibabu zaidi.
Upande wa mashitaka ulifunga ushahidi wake na katika maamuzi madogo (Ruling), mahakama ya wilaya ya Kalambo ilimuona mshitakiwa kuwa anakesi ya kujibu.
Mshitakiwa alipewa haki yake ya kujitetea na hakuwa na shahidi hivyo alijitetea yeye mwenyewe na kudai kuwa siku ya tukio alikuwa ameenda kuchota maji majira hayo ya usiku na alimuacha mtoto huyo wa siku 3 akiwa amelala ndani na aliporudi ndipo alipokuta mwanae huyo anavuja damu maeneo ya siri na alipomkagua alikuta uume wa mtoto huyo haupo na yeye hakujua nani amefanya hivyo kwa mtoto wake mpaka aliposhtuka anakuja kukamatwa na viongozi wa Kijiji wakati yeye si muhusika wa tukio hilo.
Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya wilaya ya Kalambo MH. Ramadhani Rugemalira, Ambapo alisema mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka dhidi ya mtuhumiwa.
Na wakati wa ungamo aliiomba mahakama isimpe adhabu Kali kwani yeye ni mara yake ya kwanza kuletwa mahamani na pia ana mtoto mdogo ambaye hajafikisha hta mwaka, na pia ana watoto wengine Wanne wanamtegemea.
Waendesha mashitaka kwa upande wao hawakuwa na kumbukumbu za nyuma za mshitakiwa lakini waliiomba mahakama kutoa adhabu Kali kwa mtuhumiwa kwa kuwa vitendo hivyo vimekithir katika jamiii na pia lengo la mtuhumiwa halikuwa jema.
MH hakimu kwa kuzingatia maombi ya mshitakiwa na maombi ya mwendesha mashitaka alimhukumu mshitakiwa kwa kosa la kumjeruhi mtoto wake kifungo cha nje cha miezi 12 kwa kuzingatia kifungu cha 38 cha sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 mapitio ya mwaka 2019, huku ikimuonya kutokufanya kosa lolote la kijinai ndani ya mwaka na kwa kufanya hivyo itapelekea mahakama kumpa adhabu Kali, pia hakimu alizingatia haki za watoto kwa kuzingatia kuwa mtuhumiwa ana mtoto mdogo sana na ambaye anahitaji malezi ya mama kwani mtoto huyo baba yake hajulikani alipo.
Hata hivyo nje ya mahakama baadhi ya mashirika yanayo husika na ututezi wa haki za watoto ikiwemo ECD pamoja na wananchi wameipongeza mahakamaa kwa kutoa hukumu hiyo na kuitaka kuendelea na hatua hizo za kutoa hukumu za kesi kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kupata haki zao mapema.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.