SERIKALI ya Canada kupitia Shirika lake la maendeleo (Global Affairs Canada) imekarabati miundombinu ya maji katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Rukwa na vituo viwili vya afya katika wilaya ya Kalambo na Sumbawa na kuikabidhi Serikali ya kwa ajili ya kupambana na vifo vitokanavyo na uzazi.
Aidha imekabidhi mashine maalumu za kupimia wingi wa JR5 Sdamu kwa akina mama wajawazito na mashine za kuongeza joto kwenye vyumba vya kuhifadhia watoto waliozaliwa na uzito pungufu ili kuokoa maisha yao.
Ukarabati wa vituo hivyo umetekelezwa na Serikali Canada kupitia Mradi wa Mradi wake wa Uzazi Salama Rukwa ambao unatekelezwa na mashirika matatu ambayo ni Plan Internationa, Africare na Jhpiego.
Akizungumza katika Ukumbi wa Hospitali ya Mkoa ya Rufani ya Rukwa wakati wa kukabidhi miradi hiyo pamoja na vifaa, Mkurugenzi wa Mradi wa Uzazi Salama, Gasper Materu alisema ukarabati wa miundombinu hiyo ya maji umegharimu zaidi ya shilingi milioni 542.
Materu alivitaja vituo vya afya vilivyonufaika na mradi huo kuwa ni Kituo cha Afya cha Milepa kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na Kituo cha Afya cha Matai katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.
Alisema mashine za kuongeza joto kwenye vyumba vya kulelea watoto waliozaliwa na uzito pungufu na za kupimia wingi wa damu kwa wanawake wajawazito, zilinunuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni 226 na kwamba zitagawiwa kwenye Halmashauri zote za mkoa huo.
“Hii ni ahadi yetu yetu ambayo tuliahidi kushirikiana na Serikali kuimarisha huduma za mama na mtoto, baadhi ya huduma hasa za upasuaji zinatakiwa maji ya kutosha na safi, lakini pia watoto wanaozaliwa na uzito pungufu wanahitaji mashine hizi,” alisema Materu.
Akikabidhi miradi hiyo pamoja na vifaa kwa niaba ya Serikali ya Canada, Mwakilishi wa Shirika la Global Affair Canada, Stefan Paquette alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi washirika wa Canada na ndio maana wameamua kusaidia katika afya ya uzazi.
Alisema Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayopokea misaada mikubwa kutoka Canada kwa ajili ya masuala ya afya ya uzazi ambapo alisema tangu mwaka 2010 mpaka sasa wametoa misaada isiyopungua dola milioni 292
“Mpango wa Tanzania wa mwaka 2008 mpaka 2015 ulikuwa ni kupunguza vifo vya mama na mtoto ambapo nguvu kubwa iliwekezwa kupambana na hali hiyo hivyo mpango huo unatakiwa kuendelezwa hasa katika maeneo ya vijijini ambako huduma nyingi hazifiki,” alisema Paquette.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo aliishukuru Serikali ya Canada kwa msaada huo akidai kuwa utasaidia mkoa wake kupunguza vifo vya mama na mtoto ambalo ni tatizo kubwa katika mkoa huo.
Alisema Mradi wa Uzazi Salama ambao umetekeleza miradi hiyo pia unashirikiana na Serikali ya Mkoa huo kwenye mapambano ya mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi ambazo hivi karibuni Rais John Magufuli alikemea vikali.
“Nimekuwa nikipokea taarifa za utekelezaji wa miradi hii kupitia kwa Katibu Tawala wa Mkoa akinieleza shughuli mnazofanya, nafurahi leo mnatukabidhi miradi hii pamoja na vifaa hivi, tunaomba ndugu zetu wakanada msichoke kuendelea kutusaidia,” alisema Wangabo.
Aliwaagiza wakurugenzi wa Halmashauri kwa kushirikiana na watendaji wengine kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika vizuri ili vidumu kwa muda mrefu.
Naye Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mariam Mahamood, alisema utekelezaji wa miradi hiyo utaisaidia Tanzania kufikia baadhi ya Malengo Millenia ifikapo mwaka 2030 ambayo ni suala la upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.