Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imepokea fedha kiasi cha shilingi 69,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa majosho matatu (3) ya kuogeshea mifugo ambayo yatajengwa katika kata ya Katazi, Mwazye na Mnamba hatua itakayo saidia kupunguza vifo vinatokavyo na magonjwa ya kupe, ndigana kali na baridi kwa asilimia 90.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ndugu Shafi Mpenda akiwa ofisini kwake ambae licha ya kuipongeza serikali kwa kutoa fedha hizo, amesema fedha hizo zimegawanywa katika kata tatu mbapo kila kata imepata fedha shilingi 23,000,000/= na kufanya jumla ya fedha zote kuwa million 69,000,000/=
Aidha amebainisha kuwa Miradi hiyo inatekelezwa na kampuni ya GN.&MC contraction Limited na mkandarasi amelipwa fedha shilingi 18,377,468/= kama malipo ya awali.
Kaimu mkuu wa idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Wilayani humo ndugu John Kipeta, amesema uwepo wa majosho hayo utawezesha mifugo kuwa na afya na kuwezesha wafugaji kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi.
Ameongeza kuwa uwepo wa majosho hayo utasaidia kupunguza magonjwa ya ngozi kwa asilimia 90, mkojo mwekundu magonjwa ya moyo pamoja na kudhibiti magonjwa yatokanayo na kupe.
Baadhi ya wafugaji Wilayani humo wameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kutoa fedha hizo ambazo zitawezesha kupata majosho bora na ya kisasa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.