Malalamiko hayo yamejitokeza baada ya kujitokeza kifo cha mtoto Jift Msangawale mwenye umri wa mika 3 mkazi wa kijiji cha Keleni kata ya Lyowa wilayani Kalambo kufariki dunia baada ya kuzama ndani ya kisima cha maji kilichokuwa kimechimbwa kwa ajili ya kuendeshea shughuli za umwagiliaji wa busitani za mboga mboga.
‘’tunaiomba serikali kuingilia kati swala la watu ambao wamekuwa wakichimba visima bila kufuata utaratibu kwani waliowengi wanachimba visima na kuviacha wazi na hivyo kupelekea watoto wetu kuzama’’wamesisitiza wananchi hao.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Keleni Linus leopadi,amesema baada ya kupata taarifa hizo alitoa taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi kisha kuwaruhusu kufanya mazishi.
Afisa tarafa ya Matai Muhamed Shauri amekili wazi kutokea tukio hilo na kuwataka wananchi kuhakikisha visima vyao vinafunikwa mara baada ya kuchimbwa.
‘’mtoto huyo alifariki dunia baada ya kudumbukia kisimani,ambapo kufutitia tukio hilo kama serikali tulitoa maagizo kwa watendaji wa serikali za vijiji na kata kuhakikisha visima vyote vinavyochimbwa vinafunikwa ili kuepukana na kujirudia kwa matukio kama hayo’’.alisisitiza muhamed shauri.
Hata hivyo hilo ni tukio la pili kujitokeza katika maeneo hayo ambapo tukio la kwanza watoto wawili walifariki dunia baada ya kuzama kwenye kisima kisha kufariki dunia katika kata ya Matai.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.