Naibu waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Josephat Kandege ametoa msaada wa computer katika shule zote za sekondari huku akiwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii na kutojihusisha na vitendo viovu ambavyo vinaweza kupelekea kushindwa kuendelea na masomo yao.
Akiongea na wanafunzi wa shule ya Mambwe sekondari Naibu waziri Kandege, alisema kwa kuona umuhimu wa wanafunzi ametoa computer 10 ambazo zimegawanywa katika shule tatu za sekondari ikiwemo Mambwe, Mwimbi na Matai.
Alisema baada ya corona kuisha vodacom wameahidi kufunga internet kwenye computer zote kwa muda wa mwaka mmoja na kuwasihi walimu pamoja na wanafunzi kuvitumia vifaa hivyo katika malengo kusudiwa.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Godfrey Mbwambo, alisema vifaa hivyo vitakuwa msaada kwa wanafunzi na walimu na kuahidi kuhakikisha computer hizo zinatumika katika malengo yaliyokusudiwa.
“Nampongeza sana naibu waziri kwa kutoa vifaa hivi kwani tunaimani vitarahisisha utendaji kazi kwa wanafunzi na walimu pia”. Alisema Mbwambo.
Mkuu wa wilaya ya kalambo Julieth Binyura, alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kufyatua tofali elfu ishirini kwa kila kijiji ambazo zitasaidia kongeza majengo mengine kama ilivyokuwa mwaka 2019.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.