Naibu waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Josephat Kandege ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa kuhakikisha fedha pamoja na vifaa tiba vilivyotolewa na serikali na kugawiwa kwenye vituo vya afya,vinatumika kwa melengo yaliyokusudiwa.
Ameyasema hayo wakati akitoa misaada ya vitanda pamoja na kukabidhi gari ya wagonjwa katika kituo cha afya Matai wilayani Kalambo mkoani Rukwa, ambapo ameutaka uongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha vifaa vilivyotolewa na serikali ikiwemo gari vinatumika katika malengo yalikusudiwa.
Amesema serikali haita mfumbia macho mtu au watu ambao watabainika kufuja mali za umma kwa kuingiza maslahi yao binafsi.
Awali akisoma taarifa fupi mbele ya kiongozi huyo, mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Alen Mlekwa, alisema Halmashauri ina jumla ya vituo vya afya 3 na zahanati 64 lakini inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vyombo vya usafiri magari, boti ikiwa ni pamoja na upungufu wa vifaa tiba na watumishi wa idara ya afya.
“umekuwa msaada mkubwa katika halmashauri hii na jimbo lako katika kuboresha huduma za afya, mwaka 2019 kwa kuunga mkono juhudi za huduma za afya ulitoa vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda vya wagonjwa 6, taulo 10 kwa ajili ya akina mama wajawazito seti za kumsaidia mama wakati wa kujifungua na vitambaa roll 5. Vilevile kupitia juhudi zako umetoa gari jipya la wagonjwa ambalo umetukabidhi hii leo.’’Alisema Mlekwa.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Nicholas Mrango ,alisema huduma zinazo tolewa katika kituo cha afya Matai ni pamoja na huduma ya wagonjwa wa nje yaani OPD na katika vituo vyote vya wagojwa hulazwa katika vituo 3 vya afya IPD na kusema kwa upande wa dharula kwa akina mama wajawazito hutolewa katika ngazi zote za zahanati na vituo vya afya.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura aliwasihi wahudumu wa afya wilayani humo kuendelea kuwahudumia wananchi kwa moyo wote na huku akiwasisitiza kutoa taarifakunapotokea changamoto ya kiutendaji.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.