Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na kitendo cha kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaopata ujauzito mkoani Rukwa na kuagiza vyombo vya dola na watendaji wa serikali kutekeleza sheria zilizopo ili kukomesha hali hiyo.
Alisema hayo mara baada ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo na kueleza kuwa ili mimba ziishe Rukwa kila mmoja lazima ashiriki kikamilifu katika vita dhidi ya mimba na wahusika wote wachukuliwe hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ikiwamo vifungo vya miaka 30 jela kama sheria inavyosema.
Alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mandela Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, ambapo idadi ya wanafunzi waliopata ujauzito ni 229 kwa mwaka 2018 na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo kuchukua hatua sitahiki dhidi ya wahusika wa matukio hayo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.