RC Wangabo Aingilia kati Mgogororo Waujezi Wa Kituo Cha Afya Kalambo.
Posted on: June 25th, 2019
Hatimaye mkuu wa mkoa wa Rukwa Jochochim wangabo amengilia kati mgogoro wa ujenzi wa kituo cha afya cha samazi wilayani kalambo uliomudu kwa zaidi ya miezi miwili baada kutokea kwa mvutano baina ya vijiji vinne huku kila kijiji kikitaka ujezi ufanyike sehemu yake na hivyo kupelekea uongozi wa halmashauri hiyo kusimamisha harakati za ujezi huo kwa lengo la kutafuta suruhu.
Kata ya samazi inapatikana katika mwamabao wa ziwa Tanganyika licha ya hilo kata hiyo imekuwa ikikabiliwa na chanagamoto kubwa ya ukosefu wa kituo cha afya hali ambayo imekuwa ikiwalazimu wananchi kutembea umbali wa zaidi ya km20 ili kutafuta huduma za matibabu katika kituo cha afya cha Ngolotwa.
Kwa kulina hilo serikali ilitoa fedha kiasi cha shilingi million mia nne kwa ajili ya ujezi wa kituo cha afya katika maeneo hayo na kutoa maelekezo kwa wananchi kutafuta eneo la ujezi hali ambayo ilipelekea kila kijiji kutoa mapendekezo yake na huku baadhi yao wakitaka kituo hicho kujengwa juu ya mlima na huku wengine wakiwa na mapendekezo tofauti na kupelekea uongozi wa mkoa huo kuingilia kati swala hilo.
Mkuu wa wilaya hiyo Julieth Bniyura aliwataka wananchi kufanya mamuzi sahihi juu ya eneo hilo na kuwasisitiza kuchagua eneo ambalo litakuwa na tija kwa manufa ya wengi.
ENonos Budodi mwenyekiti wa jumuhiya ya wazazi mkoani humo alisema lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanapataa huduma bora na safi kwa muda muafaka na kuwasisitiza kukubalina na maaoni yatakayo tolewa na serikali.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alisema mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe na mbomoa nchi ni mwananchi mwenyewe na kuwasihi kuendelea kufanya maendeleo katika eneo ambalo lilikuwa limechaguliwa.
Alisema selikali imetoa fedha hizo kwa lengo la kuwasaidia wananchi kuondoka na adha ya kutembea umbali mrefu wakati wa kutafuta huduma za matibabu na kusema mradi huo utatakiwa kumudu ndani ya miezi mitatu.
Kwa upande wake mkurugezi mtendaji wa hamshauri hiyo Palela Msongera alisema wamejipanga kuanza ujenzi huo mapema na kuwa tangia awali walikuwa wakisubiri mapendekezo ya eneo kutoka kwa wananchi.
Wananchi kwa upande wao waliipongeza serikali kwa kuwaunga mkono mapendekezo yao na kuwa watakuwa msitar wa mbele ili kuhakikisha wanafikia lengo.