Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewapongeza wakandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri wa ya ujenzi wa barabara ya kutoka Sumbawanga – Matai – Kasanga yenye urefu wa Km 10 7 ambayo imefikia asilimia 91 ya ujenzina kubainisha kuwa barabara hiyo imetimiza miaka tisa tangua kuanza kwa ujenzi wake lakini pamoja na mambo mengine yaliyosababisha hayo ni maelewano mabovu yaliyokuwepo baina ya Mkandarasi na Mshauri jambo ambalo hivi sasa limemalizika na kazi inakwenda vizuri.
“Mkandarasi pamoja na ‘Consultant’ hay ani matokeo ya kuelewana, ‘Consultant’ na Mkandarasi wameelewana na wanafanya kazi usiku na mchana na matokeo yake mnayaona kazi imefanyika vizuri sana mimi nawapa pongezi sana, kwahiyo mimi nategemea kama mlivyoniambi kwenye taarifa yenu kwamba kufikia tarehe 30 mwezi Septemba barabara hii itakuwa imekwishafika bandarini kasanga na tutakuwa tumemaliza mchezo lambda marekebisho ya hapa na pale,” Alieleza.
Mradi huo wa barabara ya Sumbawanga – Matai – Kasanga unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania na kugharimu Shilingi Bilioni 133.2 ambapo ujenzi wake unategemewa kumalizika mwezi Septemba mwaka 2019 chini ya Mkandarasi Joint Venture of China Railway 15G/New Century Company Ltd.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.