Watu 2,612 kutoka Mikoa 26 hapa Nchini wamenufaika na mtaala mpya ulionzishwa na Serikali kupitia wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii , Jinsia,Wazee na Watoto wenye lengo la kutoa mafunzo kwa wasaidizi wa kisheria ili kutokomeza matukio ya kikatili dhidi ya Watoto wenye umri kuanzia {0-8}
Katika kukabiliana na hali hiyo Serikali Nchini emeanzisha mkakakati wa kupambana na matukio ya kikatili wa kijinsia kwa kuanzisha madawati 408 katika vituo vya Polisi pamoja na kuongeza vituo vya mkono kwa mkono kutoka 10 hadi kufikia vituo 13 kwa mwaka 2017 na vituo13 kwa mwaka 2019.
Kaimu katibu mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto Imelda Kamugisha kupitia madhimisho ya siku ya Wanawake yaliofanyika katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa alibainisha kuwa;-
‘’Takwimu zinaonesha kuwa ukatili wa kijinsia unafanyika zaidi nyumbani na mashuleni, wanaofanya vitendo hivi vya kikatili ni aidha, ndugu wa karibu au watu wenye nafasi na mamlaka ambao badala ya kulinda Vijana na Watoto wetu wao ndio wanaleta madhara haya ya kikatili. ‘’Alisema kamgisha.
Alisema Serikali imejipanga kutofumbia macho maswala hayo hata kama itaonekana kutendwa na wanafamilia wenzao na kusihi Wananchi kutoa ushirikino ili kuwabaini wahusika wa matukio hayo .
‘’Sera ya maendeleo ya Wanawake na jinsia inasisitiza kuwepo kwa usawa na jinsia na kuendeleza Wanawake, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni pamoja na kuendelea kutekeleza mpango wa Taifa 2017\2018 –{2020\2021, mpango unaolenga kupunguza kiwango cha ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wenye umri kati ya miaka {0-8}
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo kupitia madhimisho hayo , Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Julieth Binyura, alisema mimba kwa Wanafunzi zimepungua kutoka 200 mwaka 2018 hadi 193 kwa mwaka 2019.
‘’kwa mwaka 2018 Mkoa ulikuwa na jumla ya mimba 200 kwa watoto waliopo katika Shule za msingi na sekondari ikiwa mimba 58 kwa Shule za msingi na 142 kwa Shule za sekondari. Katika kipindi cha kuanzia January 2019 hadi Desemba 2019 takwimu za mimba ziliripotiwa kwa Watoto waliopo Shule za msingi ni 50 na sekondari 143 ikifanya jumla ya mimba193 kwa Mkoa.’’alisema Binyura.
Alisema licha ya hilo Serikali kupitia Halmashauri zake umepokea taarifa ya mashauri 308 yanahusu migogoro ya ndoa na mashauri 388yakihusu matatizo matunzo ya Wat
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.