Serikali nchini imeanza uhakiki wa kaya masikini katika Halmashauri zote nchini na huku Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ikitegemea kuhakiki jumla ya Kaya 4,045 na kuziingiza kwenye mifumo.
Halmashauri ya Kalambo ina jumla ya Kata 23 na Vijiji 111, ambapo kwa kuzingatia umuhimu wa Wananchi wenye kipato cha chini imenza uhakiki wa kaya katika Vijiji 66 lengo likiwa ni kuwaondoa wanufaika hewa na baadhi ya wanufaika ambao hawana vigezo.
Mratibu wa TASAF Wilayani humo Bw. Michael Mwasumbi, amesema zoezi hilo ni muhimu kutokana na baadhi ya watu kufariki na wengine kuhama maeneo yao lakini bado wamekuwa wakitambulika kama wanufaika kituo ambacho sio sahihi.
Amesema kwa kutambua hilo Serikali imeanza kutoa mafunzo kwa watu ambao watahusika na zoezi la uhakiki na kusema uwepo wa zoezi hilo litarahisisha upatikanaji wa taarifa kwa haraka.
Kaimu meneja wa TASAF nchini Bw. Oska Maduu, amesema zoezi hilo litafanyika katika Halmashauri zote nchini na lengo kubwa likiwa ni kuwabaini wanufaika ambao hawana vigezo vya kuendelea na mradi huo,
Alisema kwa kutambua umuhimu wa zoezi hilo Serikali imeongeza mkataba wa miaka mitatu na kuwataka wanufaika wote kuzitumia fedha hizo katika malengo kusudiwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.